BODI YA KAHAWA YAINGIA KATIKA MARUMBANO

MENEJIMENTI ya Bodi ya Kahawa nchini (TCB) imeingia kwenye malumbano na uongozi wa bodi mpya ikituhumiwa kupuuza maamuzi yanayotolewa na bodi hiyo .

Miongoni mwa maagizo yanayodaiwa kupuuzwa ni kurejeshwa Makao Makuu ya bodi hiyo, Ofisa Maendeleo ya Kahawa na Mtaalamu wa kuonja Kahawa, Rogatus Meela, amehamishiwa mkoani Kigoma.

Meela ambaye ni mgonjwa, imeamuliwa na bodi mpya mapema Juni mwaka huu arejeshwe Moshi, ili awe karibu na hospitali anayotibiwa, maagizo ambayo hadi sasa hayajatekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Eve Hawa Sinare, amehoji mamlaka ambayo anayo mkurugenzi huyo ya kutotekeleza maagizo ya bodi yake.