MBEYA: HALMASHAURI YAOMBWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WAZARISHAJI WA UYOGA

HALMASHAURI ya jiji la Mbeya imetakiwa kuwajali wajasiliamali wanao jihusisha na uzalishaji wa uyoga katika usafi wa jiji kutokana na uzalishaji huo kutegemea masalia ya mimea.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake hivi karibuni
Mkuregenzi wa kampuni ya Tanmush, Gerald Mgaya amesema kuwa halimashauri ya jiji la Mbeya inatakiwa kuwajali kwani wao na
wazalishaji wengine wa Uyoga wamekuwa wakijihusisha katika utoaji wa taka katika baadhi ya masoko.

Uzalishaji huo umekuwa ukitegemea mabaki ya mimea ambayo ni makavu na kutumika kama vimeng'enywa vya uyoga.

Mgaya ambeye anakampuni pekee ya uzalishaji wa mbegu za uyoga
ukiachilia mbali chuo cha utafiti wa uyoga mkoani Mbeya.

Uyoga umekuwa ukitumia mabua ya mpunga, migomba, Mahindi ngano na mazao mengime yanayo fanana na hayo.