UGIRIKI: NI NIAKA MIWILI YA KUSIMAMA KIUCHUMI



Ugiriki itahitaji miaka mingine miwili kabla ya kusimama sawasawa kiuchumi.

Hayo ni kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Christine Lagarde.

Lagarde amewaambia waandishi wa habari mjini Tokyo kwamba muda zaidi utahitajika, ili Ugiriki iweze kukamilisha mpango wa mageuzi katika mfumo wake wa fedha.

Ugiriki ina muda hadi tarehe 18 mwezi huu wa Oktoba kukamilisha mageuzi, ili iweze kupatiwa mkopo wa euro 31.5 bilioni za kuiokoa.

Lakini Waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras amesema nchi yake haiwezi kutekeleza zaidi mpango wa kubana matumizi na kwamba hazina ya serikali itakuwa tupu ifikapo mwezi Novemba, ikiwa haikupatiwa msaada zaidi.