MFUKO WA PENSHENI WA FANIKIWA KUONGEZA PATO
MFUKO wa Pensheni (PPF) umefanikiwa kuongeza mapato yanayotokana na uwekezaji kutoka sh bilioni arobaini na tatu point arobaini na tano mwaka 2010 hadi kufikia zaidi ya sh bilioni Tisini na moja.
Hayo yalielezwa jijini hapa na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo, Dk. Adolf Mkenda, wakati akizungumza kwenye mkutano wa ishirini na mbili wa mwaka wa wanachama na wadau wa mfuko huo.
Amesema mfuko huo umeendelea kufanya vizuri, kwani katika kipindi cha Januari mpaka Juni mwaka huu mapato yatokanayo na uwekezaji yamefikia sh bilioni arobaini na saba nukta sabini na nne ambapo imevuka malengo waliyojiwekea ya kukusanya sh bilioni arobaini na saba nukta sabini na moja, katika kipindi hicho.
Mkenda amesema PPF imeongeza fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa vitega uchumi mbalimbali kutoka sh bilioni mia sita na sabini na mbilinukta mbili mwaka 2010 hadi kufikia sh bilioni mia nane mukta thelathini na saba nukta sita mwaka 2011 ambapo mfuko huo unashiriki katika ujenzi wa vyuo vikuu kikiwemo cha Teknolojia ya Sayansi ya Kompyuta kilichopo Dodoma na cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela cha jijini hapa.