MADEREVA WAOMBA NANENANEA KUWA KITUO

Chama cha madereva wa daladala zinazofanya safari kati Uyole na Stendi Kuu jijini Mbeya wameitaka serikali kufanya ujenzi wa stendi ya kudumu eneo la nanenane ili kupunguza msongamano katika stend ya Uyole.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa chama hicho Idd Ramadhani wakati wa mkutano wa kuzi jadili change moto zinazo wakabili madereva wa Daladala jijini Mbeya amesema kuwa serikali ni vema ikaliangalia suala ya kuwapo kwa stendi ya Nanenane kuwa stendi ya kudumu.

Kwa upande wake mlezi wa chama hicho mchungaji Wiliamu Mwamalanga amesema ili madereva wafanye kazi kwa uhuru lazima kutii sheria bilashariti amesema umefika wakati askari polisi kikosi cha usalama barabarani kuacha tabia ya kudai na kupokea rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.

Dereva John Mwazembe amesema manyanyaso wanayo pata kwa askari wa usalama barabarani haya paswi kufumbiwa macho
.