Wakazi wa kata ya Sinde jijini Mbeya wametakiwa kutumia vizuri lasilimali zinazopatikana katika bonde la Ilolo kata ya Sinde kwa ajili ya afya zao na kuweza kujipatia kipato cha kila siku.
Wito huu umetolewa na mwenyekiti wa kata ya Sinde, Bw. Ambwene Mwasongwe na amewataka wananchi wanaotumia bonde hilo kusafisha mifereji ya maji iliyopo bondeni hapo ambayo ndiyo inayotumika katika umwagiliaji wa bustani za mbogamboga.
Wakizungumza na Rock Fm wananchi wa maeneo hayo ya vyanzo wamesema wataacha kutupa taka mbalimbali ikiwemo mizoga ya wanyama katika vyanzo hivyo hali ambayo inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa, kwani maji hayo hutumika pia kwa shughuli za nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)