WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, ameitaka Tume ya Ushindani nchini (FCC), kuhakikisha inalimaliza haraka tatizo la bidhaa bandia zilizozagaa mitaani kwani ni aibu kwa serikali.
Dk. Kigoda ametoa agizo hilo amefanya ziara ya kufahamiana na wafanyakazi wa tume hiyo pamoja na Baraza la Ushindani (FCT).
Katika ziara hiyo ambayo ameambatana na naibu wake, Gregory Theu, amesema jamii imekuwa ikiitupia lawama serikali kuhusu bidhaa hizo kutokana na tume hiyo iliyokabidhiwa jukumu kutojulikana kazi zake kwa jamii.
Kwa upande wa FCT, Kigoda ametoa wito kwa watendaji kuwa wabunifu katika kutafuta njia zitakazowafanya watambulike katika jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)