WILAYA ya Kyela Mkoani Mbeya inatarajia kuunda bodi ya kokoa kwa ajili ya kuongeza tija katika ununuzi wa zao hilo kutoka kwa wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Kyela, Bi. Magret Malenga amesema kuwa amekaa na maafisa ushirika wilayani humo na kuunda kamati itakayo shughulikia uundwaji wa bodi ya kokoa.
Amesema kuwa anaumia kuona wakulima katika wilaya yake wakiteseka katika kutafuta masoko na uamuzi wa kuundwa kwa bodi hiyo kutasaidia kuleta tija kwa wakulima wa kokoa wilayani humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)