WAKULIMA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA KILIMO

WAKULIMA wilayani Mbozi mkoa ni Mbeya wametakiwa kutoa ushirikiano na kwa maafifa kilimo ili kupambana na pembejeo ambazo hazifai.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa kilimo wilayani Mbozi wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kunyang'anywa kwa leseni ya uuzaji wa mbolea ya kampuni inayo jihusisha na uuzaji wa mbolea wilayani humo ya Stako kutokana na kuuza mbolea isiyofaa kwa kilimo na kutoleta mabadiliko katika mazao.

Mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea, Dakta amesema kuwa kampuni ya Stako imesimamishwa kuendelea na usambazaji wa mbolea wilayani humo.