WAZAZI wanatakiwa kuwa makini na waangalizi wa zuri katika
kuvitambua vipaji vya watoto wao na kuviendeleza ili viwasaidie baadae katika
maisha yao.
Akizungumza katika maafari ya sita ya darasa la saba yaliyo
fanyika hivi karibuni katika shule ya St.Mary’s ya mkoani Mbeya na Afisa tawala
wa shule hiyo, Anuciatha Ngonyani alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa vikwazo
katika kuendeleza vipaji vya watoto wao.
Alisema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwazuia watoto wao
kushiriki katika mambo mbalimbali ya kuonyesha vipaji vyao hasa katika Michezo
ya aina tofauti na huku mtoto akiwa na kipaji cha kujeza na anaweza.
Ngonyani amewataka wazazi kuwa ruhusu watiti wao kushiriki
katika michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu ambapo kwa ulimwengu wa sasa ni
ajira ambayo imakipato kikubwa ambacho baadhi ya marais wapo chini zaidi ya
wachezaji wa mpira.
Kwa upande wa wanafunzi katika risara yao wamesema kuwa
wanaomba waboreshewe viwanja vya michezo ili waonyeshe vipaji vyao walivyo
navyo na kuahidi kufanya vizuri katika
mtihani wao wa darasa la saba.
Walisema wakiboreshewa viwanja hivyo vitawasaidia katika
michezo mbalimbali ya hapo shuleni hapo ambayo imebainika kuna wanafunzi wengi
wenye vipaji vya kimichezo.
Nae mgeni Rasmi katika maafari hayo, Haji Seliman Control wa
CRDB tawi la Mbeya kwa niaba ya Meneja, alisema kuwa suala la michezo mashuleni
ni muhimu sana katika kwa wanafunzi na humsaidia mtoto katika kuboresha akili
yake kwani nichezo ni afya na baadae kuwa ajila yenye ujila mkubwa.
Seleman kwa kuhakikisha wanafunzi wana tumia fulsa vizuri ya
kuonyesha vipaji vyao alimkabidhi afisa tawala wa shule hiyo Bi Ngonyani mipira
mitatu ya kuchezwa kwa miguu na kuwataka wa wajitahidi kuwaonyesha vipaji vyao.
Alisema ombi la wanafuzi hao amelipokea na kulifikisha
katika uongozi wa CRDB na kuitazama bajeti yao na huenda wataboresha viwanja
vya nichezo au kuvijenga upya kulingana na bajeti yao itakavyo kuwa.
Seleman alimpa afisa tawala wa shule hiyo kazi ya kufanya
tathimini ya ghalama za uboreshaji wa viwanja vivyo ili vianze kuboreshwa na
kuwafanya wanafunzi kufurahia michezo na kuonyesha uwezo wao katika viwanja
bora vya michezo yao.
