SERIKALI katika kukabiliana na matatizo ya kuwapitisha
wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika kuingia katika kidato cha kwanza mwaka
huu waalimu wa kuu wa shule hawata ruhusiwa kusimamia mitihani badala yake
kusimamiwa na msimamizi mkuu pekee.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwa na wanafunzi wengi wanao
pasi na huku hawajui kusoma wala kuandika njia hii itasaidia kupunguza ama
kuondoa kabisa suala hilo la kuwapo kwa wanafunzi wasio jua kusoma wa kuandika
katika kidato cha kwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari afisa elimu wa Mkoa wa Mbeyu Juma kaponda hivi karibuni
alisema kuwa ili kupambana na tatizo hilo ambalo ni changamoto kubwa kwa taifa
ni vyema waalimu wakuu wakaondolewa katika usimamizi wa mitihani ya wanafunzi
wao.
Suala
la mwanafuzi kuingia kidato cha nne akiwa hajui kusoma wala kuandika si aibu
kwa taifa bali ni changamoto kwa taifa na ibidi kukabiliana nayo.
“Suala hilo la wanafunzi kuingia katika kidato cha kwanza
wakati hajui kusoma na kuandika ni si aibu kwa taifa bali ni changamoto ambayo
taifa lina bidi kukabiliana nalo na katika kukabiliana changamoto hiyo waalimu wakuu
hawata husika katika usimamizi wa wanafunzi wao,” alisema Kaponda.
Kaponda alisema kuwa waalimu walio simamia mikondo ambayo
ilitoa wanafuzi ambao hawajuu kusoma wala kuandika wamesimamishwa katika zoezi
zima la usimamizi wa mitihani ya darasa la saba kwa kipindi cha miaka mitatu.
Hatua ambayo serikali mpaka sasa imeichukua kwa sasa ni
kuhakikisha inawatambua wanafuzi wote ambao mpaka wanaingia darasa la saba
hawajui kusoma wala kuandika majina yao yataandikwa na wakuu wao wa shule mpaka
anaingia katika chumba cha mtihani serikali itajua shule Fulani mwanafuzi A
hajui kusoma wala kuandika watamuangalia mpaka wakati wa kusahisha mtihani wake
wa taifa.
Hii itaisaidia serikari kujua katika halmashauri Fulani kuna
wanawanafuzi kadhaa ambao hawajui kusoma wala kuandika na kama watafauru
serikali itajihoji kwanini wamefauri na kama ameoteha hawawezi kuwa wengi waliootea.
Yeyote atakasesima chumba cha darasa ambacho kitatoa
mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika kabla hajaenda sekondari atabainika na
mwalimu aliye simamia chumba hicho atachukuliwa hatua atachukuliwa hatua za
kisheria.
Aidha Kaponda alisema kuwa serikali kwa mwaka huu wanafunzi
wa darasa la saba wata jaza majibu yao katika karatasi maalum ambalo
litaiwezesha mashime kusaisha mitihani hiyo hii itasaidia kuepusha makosa
madogo madogo katika usahishaji na kupunguza muda wa usahishaji wa mitihani.
Kaponda ametoa wito kwa wasimamizi wa mitihani na kusema
kuwa mitihani ni vita kati ya mtahini na mtahiniwa, msimamizi akiwa anatoka nje
mara kwa mara atamsababishia mwanafuzni kuingia katika vishawi vya kufanya
udanganyifu.
