HATARINI KUPATWA NA NJAA

ASILIMIA 20 hadi 30 ya kaya za Wilaya ya Kongwa, zipo hatarini kukumbwa na njaa katika kipindi cha mwaka 2012/13.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Athumani Akalama, hali hiyo inatokana na ukame ulioikumba wilaya hiyo katika kipindi cha Januari hadi Februari, mwaka huu.

Akalama amesema mazao karibu yote yaliathirika, lakini kwa viwango tofauti, huku akisema mahindi yaliathirika zaidi kwa wastani wa asilimia 30, mtama kwa asilimia 5, alizeti na mazao ya jamii ya mikunde kwa asilimia 15.

Kufuatia hali hiyo amesema katika kipindi cha Machi mwakani upungufu wa chakula katika kaya zenye kipato cha chini utaongezeka.