MKUU wa Wilaya (DC) ya Sikonge, mkoani Tabora, Hanifa
Selengu, amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa madai ya
kushindwa kuwajibika katika majukumu yake ikiwemo kutofuata maagizo yake.
Selengu amemuweka ndani Ofisa Utumishi Msaidizi wa
halmashauri hiyo, Elly Arkechi kwa siku moja akimtuhumu kukwamisha kazi yake.
Tukio hilo lilitokea katika kikao cha kamati ya sherehe na
maandalizi ya mbio za mwenge wa uhuru na Arkechi, amesema ni kweli alilala
ndani saa 24.
