MGOGORO wa ujenzi wa kituo cha wazee cha Tunaini la wazee
Tanzania Tuwata limechukua sura mpya baada ya uongozi wa asasi hiyo kumuandikia
mkurugezi wa jiji la Mbeya ili kupata ufafanuzi.
Akizunguza na Rock Fm
mwenyekiti wa asasi hiyo Dr. David Magogo amesema kuwa wameamua kuchukua hatua
hiyo baada ya kumuandikia mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Jumanne Iddy, ni
kutokana na kuto rizika na barua walizo kuwa wakizipokea kutoka katika ofisi
yake.
Amesema katika barua hiyo ambayo wamemtumie moja kwa moja
mkurugenzi na kuambatanisha na barua za awali ambazo waliomba kibali cha ujenzi
wa kituo hicho cha huduma kwa wazee, ambazo zikiwa na mkanganyiko mkubwa wa
kuruhusu na kubadilisha ombi lao la ujenzi.
Tangu julai 27 mwaka huu takribani mwezi mmoja sasa bado
hawaja pokea majibu ya barua yao na kuwa Dr. Magogo na wenzake watafika katika
ofisi yake kufuatilia majibu ya barua yao.
