CHAMA cha waandishi Mkoani Mbeya kifikia azimio la kuto
jishughulisha na habari za kipolisi hadi jeshi hilo litakapo wachukulia hatua
wahusika wa tukio hilo na kuhakikisha kuwalinda waandishi wa habari katika
matukio ya hatarishi na kutoa utatuzi kufuatia kifo cha Mwandishi wa habari wa
Iringa.
Mbali ya kuandika habari zitokazo katika katika jeshi hilo
waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya wamepokea kwa masikitiko makubwa na
kulaani kitendo kilicho fanywa na Jeshi la polisi Mkoani Iringa na kuikana tume
iliyo undwa na jeshi hilo kufanya uchunguzi kuhusiana na tukiohilo.
Wana habari wamependekeza kuwa tukio hilo uchunguzi wake
ufanye na watu kutoka nje ya jeshi hilo wakiwemo waandishi wa habari.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Mwenyekiti
wa Mbeya Press Club, Christopher Nyenyembe amesema kuwa Mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa katika
jiji la Mbeya wilayani Rungwe na
taratibu za maziko zinafanyika huo mkoani Iringa.
Marehemu alikuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten, Daud
Mwangosi, mkoani Iringa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani
humo.
