SYRIA: VIWANJA VYA NDEGE VYASHAMBULIWA

Waasi nchini Syria leo wamevishambulia viwanja vya ndege viwili vya kijeshi katika mkoa wa Kaskazini wa Idlib.

Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa waasi wameharibu kiasi cha helikopta tano na zaidi ya ndege sita za kivita aina ya F16 katika viwanja vya ndege vya Taftanaz na Abu al-Zouhour.

Wanajeshi wa serikali mepema leo waliyashambulia maeneo yaliyo karibu na viwanja hivyo vya ndege, kulingana na shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Syria. 


Waandamanaji usiku kucha waliingia barabarani katika mikoa ya Idlib na Aleppo, na maeneo ya katikati ya Hama na Homs wakibeba mabango dhidi ya Rais Bashar al-Assad, ambaye aliapa kuendelea kupingana na kuwaangamiza waasi. 

Wakati huo   huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameitaka Iran kusaidia hali nchini Syria Naye Rais wa Misri, Mohamed Morsi, akiihutubia mkutano wa kilele wa nchi zisizofungamana kwa upande unaoendelea mjni Tehran, alisema ni lazima nchi zite zitambue umwagikaji damu unaoendelea Syria na hawawezi kusitisha hilo bila ya kushirikiana.