IRAN HAITA ACHA HAKI YAKE KUTENGENEZA NISHATI YA NYUKRIA


Kiongozi mkuu wa  Iran Ayatollah Ali Khamenei ameuambia mkutano wa kilele wa nchi zisizofungamana na upande wowote ulioanza leo mjini Tehran kuwa, Iran haitengenezi silaha za nyuklia, na haitaacha haki yake ya kutengeneza nishati ya nyuklia.

Khamenei ameyataja matumizi ya zana za nyuklia na silaha nyingine za uharibifu mkubwa kuwa ni "dhambi kubwa isiyoweza kusamehewa".

Akizungumzia vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na nchi za magharibi ili kuishinikiza Iran kuhusiana na suala hilo la nyuklia amesema vikwazo hivyo havitaathiri mipango ya nchi hiyo tu, bali vimerahisisha juhudi zake na kuimarisha matumaini yake.