MOSHI: RAIA AKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA (UNGA)

POLISI mkoani Kilimanjaro, wamemtia mbaroni raia wa Lithuania, Kristina Biskasevskaja (20), akiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa kilogramu 4.4.

Mtuhumiwa huyo mwenye hati ya kusafria iliyotolewa Agosti 7 mwaka huu, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimatiafa wa Kilimanjaro (KIA), akisafiri na ndege ya Shirika la Ndege la Eithiopia akielekea nchini Ubelgiji kupitia Eithiopia.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mwimbaji, alikuwa ameficha dawa hizo ndani ya begi lake la nguo.

Amesema baada ya maofisa wa polisi wa uwanja wa ndege kumtilia shaka, wakamkamata na kumfanyia upekuzi na kubaini kuwapo kwa dawa hizo.