MBEYA LEO: MAMILIONI YATENGWA UJENZI WA VYOO

Zaidi ya milioni 100 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya jumuika katika sehemu mbalimbali za halmashauri ya jiji la Mbeya ikiwa ni pamoja na kwenye masoko.

Akizungumza na Rock Fm Mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Jumanne Iddy amesema kuwa halmashauri ya jiji la Mbeya  limetenga fedha zaidi ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya kujenga vyoo vya kulipia katika masoko mbali mbali, stendi na maeneo ya Uhindini.

Iddy amesema kuwa kwasasa katika stendi kuu tayari Halmashauri imeisha kamilisha choo na katika soko la Soweto ujenzi unaendelea na katika masoka ya Uyole na Ilomba ujenzi unaendelea.