TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya kufuatilia utekelezwaji wa miradi ya LVEMP II (TCSD), imesema miradi mingi ya kijamii ya kudhibiti uhalibifu wa mazingira ya bonde la Mto Simiyu na Ziwa Victoria imeshindwa kutekelezwa vema kutokana na ucheleweshwaji mkubwa wa fedha na mabadiliko ya tabianchi.
TCSD imesema changamoto hizo zinatakiwa kufanyiwa kazi na idara husika, ikiwa ni pamoja na serikali kupitia idara inayosimamia miradi ya LVEMP II kuhakikisha inapeleka fedha kwa wakati kwenye vijiji na vitongoji vinavyotekeleza miradi hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Utawala na Fedha wa taasisi ya TCSD nchini, Godwin Kalokola, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kirumba jijini Mwanza.
Amwsema miradi mingi ambayo ipo chini ya utekelezwaji wa LVEMP II ambayo imeibuliwa na wananchi wa vijiji vinane wilayani Magu mwaka 2011, imeshindwa kufikia malengo kutokana na changamoto ya ucheleweshwaji fedha na ukame.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
