MBEYA LEO: WANANCHI WATAKIWA KIJITOKEZA KUCHANGIA DAMU

WANANCHI mkoani Mbeya  wameombwa kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji wa damu katika kituo cha damu salama kilichopo hospitali ya wazazi Meta jijini Mbeya .

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa kitengo cha damu salama Bw Saria Kundaeli wakati akizungumza na Rock Fm amesema kuwa kwa sasa kuna upungufa wa damu katika kituo hicho kwani kuna jumla ya lita elfu 18 tu kiasi ambacho ni kidogo kwani lita zinazo hitajika kwa mwaka ni lita elfu 24 za damu katika mikoa ya nyanda za juu kusini .

Hata hivyo amefafanua kuwa damu inatumika kwa kwa akina mama wajawazito ambao hujifungua kwa kupasuliwa watu walio pata ajali na kupoteza damu nyingi ikiwa ni pamoja na magonjwa mengine yanayo mfanya mtu kuishiwa damu na hadi sasa hakuna upatikanaji wa damu zaidi ya kupatikana kwa binadamu hivyo anawaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchangiaji wa damu.

Kundaeli amesema kuwa uchangiaji wad au una husisha watu wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 65 na wenye afya njema katika zoezi hilo na amewaomba wazazi kuwahimiza vijana wao kuhusiana na zoezi la uchangiaji wa damu kwani zipo faida nyingi ikiwa ni pamoja na kujua afya yake kwa kupimwa magonjwa mbalimbali na group la damu yako na zoezi la hilo ni bure .