IKIWA zimebakia siku chache kuanza kwa zoezi la sense ya
watu na makazi wananchi wa kata ya Kiwila wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wameshauriwa
kujiepusha na maneno mbalimbali yanayo ibuliwa na baadhi ya viongozi wa siasa ambao
hawaoni umuhimu wa zoezo hilo.
Akizungumza na Rock Fm Diwani wa kata ya Kiwila Laulent
Mwakalebule amesema kuwa pamoja na kwamba vyombo malimbali vya habari Radio
Television na magazeti vinatangaza kuhusu mambo ya sensa baadhi ya wananchi wa
kiwila hawaoni umuhimu wa zoezi lenyewe na kulichukulia vibaya zoezi hilo.
Hata hivo amesema kuwa watu wengi bado hawaja patiwa elimu
kuhusiana na sensa kwani hiyo inatokana na takwimu kuchukuliwa na kucheleweshwa
kutolewa kwa majibu.
Aidha mwakalebule ametoa tahadhali kwa wananchi kujitokeza
kwa wingi ili wahesabiwe kwa ni takwimu na makazi ni muhimu kwa taifa.
