BARAZA la Watumiaji wa Huduma za Sumatra limesema
litazishtaki daladala zitakazoshiriki mgomo ulioitishiwa na Chama cha Wamiliki
wa Daladala Jijini Dar es Salaam (Dacoboa).
Kauli hiyo ya baraza imekuja baada ya Dacoboa kutishia
kugoma kwa madai kuwa Sumatra imekuwa ikitumia ulinzi shirikishi kuwakamata.
Katika hilo, katibu mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo, amesema
mgomo ambao umeitishwa na Dacoboa ni batili kwa sababu kulingana na kanuni za
udhibiti, chama hicho hakina mkataba na wala si mtoa huduma wala hakidhibitiwi
na Sumatra.
