WANANCHI wa kijiji cha Shai kilichopo kata ya Mlangali
wilayani Mbozi wamehuizunishwa na kitendo cha kunyang’anywa kwa ardhi ya mzee
Mwamlima sababu kubwa ikiwa ni ya kisiasa.
Kwamujibu wa Afisa mtendaji wa kijiji cha Shai Bw Patrick
Mkea amesema wajumbe watano ndio wanao fanya fujo na kunyang’anya mzee huyo
ardhi kinyume na taratibu, hata hivyo mkutano walio ufanya wajumbe hivi
karibuni ulikuwa ni kinyume cha taratibu kwa sababu hawakuwashirikisha wajumbe
wa baraza la ardhi.
Hata hivyo kikao ambacho kimehudhiliwa na viongozi
mbalimbali wa kata ikiwemo baraza la ardhi la kata na baraza hilo la ardhi
wamedai kuwa mzee Mwamlima hana kosa bali taizo hili ni la kisiasa.
Aidha uongozi wa ardhi umetoa wito kwa tatizo la ardhi
lisewa linapelekwa kwenye ofisi za kata kabla ya kupelekwa katika ofisi za
baraza la ardhi kwa utatuzi.
