WATU
wawili wanaosadikika kuwa ni wahusika wa kifo cha binti mmoja aliyeuawa
kwa kuchomwa na kisu eneo la Nzovwe Jijini Mbeya kwa kile kinachadaiwa
kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi wamekamatwa na Jeshi la Polisi.
Habari
zilizotufikia hivi Punde, zimesema kuwa wanaume hao wawili
wanashikiliwa kwa mahojiano ambapo mmoja inaelezwa kuwa ndiye
aliyehusika na mwingine ni anayedaiwa kuwa alikuwa na mahusiano mapya
na marehemu.
Taarifa
kamili kikosi kazi cha mtandao wa kalulunga kinafuatilia na baada ya
kukamilisha uchunguzi kitazianika hapahapa mtandaoni.
