SOMALIA: SITA WAUAWA NA NDEGE ISIYO NA RUBANI

Ndege ya kigaidi isiyo na rubani ya Marekani imeua raia wasiopungua sita kusini mwa Somalia.

Walioshuhudia wanasema hujuma hiyo imefanyika Jumatano asubuhi karibu na kisiwa cha Kuda ambapo raia sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Kwa muda mrefu sasa Marekani imekuwa ikitumia ndege zisizo na rubani kushambulia raia huko Pakistan, Afghanistan, Yemen na Somalia kwa madai ya kukabiliana na wanamgambo wa al Qaida.

Hata hivyo Waislamu wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulio hayo ya Marekani. Umoja wa Mataifa umelaani hujuma ya ndege hizo za kigaidi za Marekani na kusema ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.