IRANI: ANNAN ANATUMAINI KUUNGWA MKONO MPANGO WA KUSITISHA MGOGORO WA SYRIA
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu kwenye mzozo wa Syria, Koffi Annan, amewasili nchini Iran, ambako atajadiliana na viongozi wa nchi hiyo kuhusu mgogoro wa Syria.
Annan anatumai Iran itaunga mkono mpango wake mpya unaolenga kukomesha mgogoro huu uliyodumu kwa mizi 16 sasa.
Ziara ya Annan mjini Tehran inafuatia mazungumzo aliyoyafanya na rais Bashar al-Assad mjini Damascus jana.
