THE HEGI: JELA MIAKA 14 MBABE WA KIVITA WA DRC- CONGO



Mahakama ya kimatifa ya uhalifu, ICC, ya mjini The Hegi, Uholanzi imemhukumu kufungo cha miaka 14 jela, mbabe wa kivita wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Thomas Lubanga.

Lubanga mwenye umri wa miaka 51, alitiwa hatiani mwezi Machi mwaka huu, kwa kosa la kuwatumikisha watoto jeshini walio chini ya umri wa miaka 15. Makosa hayo aliyatenda kati ya mwaka 2002 na 2003.

Hata hivyo, Jaji anayesimamia kesi hiyo, Adrian Fulford, amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha tuhuma za unyanyasaji wa ngono dhidi yake.