DODOMA: ELIMU YA SEKONDARI YA KITANZANIA HAITOIFULSA YA AJILA KWA WAHITIMU



IMEELEZWA kuwa tatizo kubwa linalowakabili vijana na taifa katika suala zima la ukosefu wa ajira nchini ni kutokana na wengi wao kuwa na tabia ya kuchagua kazi za kufanya.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa (CHADEMA) Cecilia Paresso kwenye mdahalo wa kujadili tatizo la ajira kwa

vijana ambao umeoandaliwa na Taasisi ya Tuzo ya kitaaluma Tanzania(TAAA).

Paresso amesema kuwa tatizo la ukosaji ajira kwa vijana nchini limekuwa ni sugu kutokana na mfumo wa elimu uliopo nchini

ambao haumsaidii kijana aliyemaliza shule ya sekondari au chuo kujiajiri mwenyewe.

Amesema mfumo wa elimu inayotolewa hapa nchini humdumaza mwanafunzi na kumfanya afikirie kuwa atakapomaliza elimu

yake ni lazima aajiriwe na serikali, kitu alichodai kuwa si kweli.