Watetezi wa haki za binadamu wamepokea vyema mpangokazi wa Serikali ya Mpito ya Shirikisho ya Somalia uliotiwa saini hivi karibuni wa kuacha kuandikisha askari watoto.
TFG ilitia saini mpangokazi huo tarehe 3 Julai katika mkutano wa
Kikundi cha Mawasiliano cha Kimataifa kwa Somalia huko Roma, ikiapa
kuchukua hatua za muhimu kuacha kuandikisha askari watoto katika jeshi
la taifa. Uridhiaji kamili utasababisha kuifuta Somalia katika orodha
ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya vikundi ambavyo vinavyoajiri
askari watoto, ambayo ameikuwepo tangu 2007.
Katika Mpangokazi huo, serikali ya Somalia ilikubali kuwarejesha
katika jamii watoto waliotolewa jeshini na kuwaingiza asasi za kijamii
kwa msaada wa Umoja wa Mataifa. Mpangokazi huo pia ulijumuisha ufanyaji
wa kosa la jinai kuandikisha askari watoto katika sheria za taifa na
kutoa ufikaji usiozuilika wa Umoja wa Mataifa kwenye taasisi za jeshi
kuthibitisha uridhiaji huo.
Saini ya serikali kuhusu mpangokazi ni hatua ya ukaribisho mzuri,
alisema Abdullahi Mohamed Hassan, mkurugenzi wa Mogadishu Media House,
ambao ni amilifu katika kuhamasisha amani na kutetea haki za waandishi
wa habari.
"Tunahimiza Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) kuchukua hatua
muhimu kulinda watoto dhidi ya uandikishaji askari na kufanya kazi
kuelekea kwenye uachiaji wa watoto wote ambao wanafanya kazi katika
vikosi vya jeshi, pamoja na urekebishaji upya wa askari mtoto,"
aliiambia Sabahi.
"Pia tunatoa wito kwa mamlaka zinazohusika kutoa miradi ya maendeleo
kuunganisha upya watoto ambao waliandikishwa askari kwa njia ya elimu,
msaada wa kisaikolojia na kijamii, mafunzo ya utaalamu, na utoaji wa
fursa za kazi," Hassan alisema. "Wakati huohuo, taratibu muhimu lazima
zichukuliwe kuhitimisha tukio hili la kuandikisha askari watoto katika
vikosi vya jeshi."
Hassan alielezea kitendo cha kuwaajiri watoto na kuwatumia kama
askari kuwa ni "ukiukwaji unaosikitisha sana ambao watoto wamefanyiwa,
pamoja na ukiukwaji wa sheria ya kimataifa."
"Ni uharibifu wa kimwili na kiroho kwa watoto, ndiyo maana utaratibu huu hauwezi kuvumiliwa," alisema.
Abdi Adawe Ali, mwenyekiti wa Shirika la Haki za Watoto, alisema
kwamba hii ni mara ya kwanza kwa Somalia kujiunga na nchi nyingine
kupambana na kuwaajiri watoto wanajeshi. "Ni muhimu sana kwamba TFG
kuheshimu ahadi zao na ukosaji wa kuwaajiri watoto wanajeshi," alisema.
"Mpangokazi uliosainiwa ni hatua muhimu katika kumaliza ajira kwa
wanajeshi watoto na tunatoa wito kwa serikali kutafsiri mpango huu
katika taratibu zinazoshikika ambazo zinatekelezwa katika ngazi ya
chini," aliiambia Sabahi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
