WAWILI WAFARIKI WAKIWA KWA MGANGA WA KIENYEJI

WANAWAKE watatu wa familia moja, wamejikuta wakizirai kwa zamu baada ya kunyweshwa dawa na mganga wa kienyeji ‘Sangoma’ walikokwenda kupiga ramli katika Kitongoji cha Mikocheni, kijiji cha Namambo, kata ya Totowe, wilayani Chunya, Mbeya.

Tukio hilo lilitokea Julai mosi mwaka huu, ambapo wanawake hao walikwenda kwa mganga huyo aliyefahamika kwa jina moja, Lushinga, kwa lengo la kuagua wakitaka kufahamu kwa nini mama yao mwenye miaka 75 haoni na anasumbuliwa na ugonjwa wa macho kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka kijijini hapo zilisema kuwa baada ya kunyweshwa dawa na mganga huyo, wanawake hao walizirai mara moja na kuzinduka baada ya siku tatu saa saba mchana huku wakiwa hoi kwa uchovu.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namambo, Zacharia Mwandanji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja wanawake hao kuwa ni Emaculate Gibson, Tatu Gibson na Nampomwa.

Imani za kishirikiana zimekuwa chanzo cha mauaji mengi mkoani hapa, tabia ambayo imelaaniwa vikali na asasi mbalimbali ikiwemo ya Muungano wa Jamii Tanzania (MUJATA)