MBEYA: MWANAFUNZI AFARIKI DUNIA KUWA KUGONGWA NA GARI
MWANAFUNZI wa Shule ya msingi Sinde amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari huko mtaa wa Makunguru Shule ya mkapa mkoani hapa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athumani amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12:00 jioni na kumtaja marehemu kuwa ni Rugano Anyosise mwenye miaka mitano.
Kamanda Athumani ametaja chanzo cha ajali kuwa ni mtoto huyo kucheza barabarani na kuwa dereva wa gari hilo alikimbia Baada ya ajali hiyo kutokea.
Aidha kamanda Athumani ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwa maeneo wanayocheza watoto yawe salama ili kuepusha ajali zisizo za lazima.pia ameongeza kuwa dereva wa gari hilo anatafutwa na jeshi la polisi ili kujibu tuhuma zake.
