MBEYA: WAKAZI WALILIA MAJI

WAKAZI wa Kijiji cha Ilota kata ya Mshewe halimashauri ya Mbeya wameiomba serikalai kuwatatulia tatizo la maji ambalo limekuwa likiathi uchumi wao.

Wakizungumza na Elimtaa wakazi wa kijiji hicho kilichopo katika kata ya Mshewe wameiomba serikali kutoa huduma hiyo kama itolewavyo katika kata na vijiji vjingine hapa nchini.

Mwenyekiti wa kikundi cha Zinduka Bi. Witness Sikayangacha kijijini hapo amesema wanaiomba serikali kufanya hivyo ili wakazi wa kijiji hicho kuwa kama watanzania wengine wanao pata huduma bora.

Amesema mbali na kukosa maji katika kijiji hicho cha Ilota pia katahiyo imekuwa na upungufu wa huduma mbalimbali za afya.