Ukuaji wa uchumi wa China umepungua na kufikia kiwango cha
chini katika muda wa miaka mitatu katika robo ya hivi sasa ya
mwaka huu, wakati mauazo ya nje na uwezo wa watumiaji
ukidhoofika.
Data zilizoripotiwa leo zinaonyesha kuwa uchumi huo wa pili kwa ukubwa duniani umeongezeka kwa asimilia 7.6 katika miezi mitatu iliyomalizikia Juni, ikiwa ni chini kutoka asilimia 8.1 katika robo iliyopita ya mwaka huu.
Huo ni ukuaji wa taratibu mno tangu robo ya kwanza ya mwaka 2009 wakati mzozo wa kifedha duniani ulipokuwa ukiendelea.
Ongezeko la bidhaa zinazouzwa nje limepungua taratibu huku kukiwa na matatizo ya mahitaji duniani na uwezo wa wawatumiaji nchini China umedhoofika.
Serikali imepunguza riba mara mbili tangu mwanzoni mwa mwezi Juni na kuanzisha hatua kadhaa za kuchochea ukuaji wa uchumi.
Wadadisi wa masuala ya kiuchumi wanatarajia ukuaji wa uchumi kurejea tena katika hali yake ya kawaida katika sehemu ya pili ya mwaka huu lakini mdororo wa uchumi unaongeza kitisho cha upotevu wa nafasi za kazi pamoja na kuleta wasiwasi wa kisiasa.