SYRIA: WATU WAUAWA JANA

Kundi  la  wanaharakati  nchini  Syria  limesema  kuwa  yamefanyika mauaji  mapya  jana  katika  jimbo  la  kati  la  Hama. 

Uongozi  wa baraza  la  mapinduzi  la  Hama  umeliambia  shirika  la  habari  la Reuters  kuwa  kijiji  kinachoishi  Waislamu  wa  madhehebu  ya Sunni  cha  Taramseh  kilishambuliwa  kwa  helikopta  za  kijeshi pamoja  na  vifaru  na  kwamba  wanamgambo  wanaoiunga  mkono serikali  wa  kabila  la  Alawii   baadaye  walivamia  kijiji  hicho   na kufanya  mauaji  ya  kikatili. 

Idadi  ya  watu  waliouwawa inakuwa vigumu  kuithibitisha  nchini  Syria, nchi  ambayo  serikali  inazuwia waandishi  habari  kwenda  katika  maeneo  mbalimbali. Wakati  huo  huo, mjini  New York, baraza  la  usalama  la  umoja  wa mataifa  linaendelea  kuvutana  kuhusiana  na  azimio  kuhusu  hali ya  baadaye  ya  ujumbe  wa  umoja  wa  mataifa  nchini  Syria ambao  umeingia  katika  mzozano. Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani  na  Ureno  zinataka  azimio  ambalo  litaweka  muda  wa siku  kumi kwa  Assad kusitisha  mashambulizi  yake ama  akabiliwe na  vikwazo  chini  ya ibara  ya  7  ya  mkataba  wa  umoja  wa mataifa. 
Urusi  inakataa madai  ya  mataifa  ya  magharibi  ya vikwazo.