UGIRIKI: SASA NI MAANDALIZA YA KUANDAA SERIKALI


Washindi wa uchaguzi wa bunge nchini Ugiriki wanasema wanajiandaa kuunda serikali ya mseto na Wasoshalisti hii leo.

Hatua hiyo itaviruhusu vyama viwili kugawana madaraka licha ya kura muhimu ya kuupinga utawala wa nchi hiyo.

Antonis Samaras, ambaye chama chake cha New Democracy kilipata ushindi mdogo, alikutana jana na viongozi wa chama cha Kisoshalisti cha PASOK.