MHASIBU
MKUU wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Fedinand Nanyele
anakabiliwa na shutuma za ubadhilifu wa fedha za miradi zaidi ya Sh.
Milioni 100.
Taarifa
za uchunguzi zilizothibitishwa na baadhi ya idara nyeti za Serikali
zilisema kuwa mwasibu huyo baada ya kuhusishwa na ubadhilifu huo
alikamatwa na kuhojiwa na taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa mkoani
Mbeya na anatarajia kufikishwa mahakamani hivi karibuni.
Mbali
na Mhasibu huyo, tuhuma hizo pia zinamhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa
wilaya hiyo George Kagomba ambaye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa
matumizi ya fedha hizo za miradi ya Afya na ujenzi wa majengo ya
Sekondari wilayani humo.
Akithibitisha
tuhuma hizo, Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka alisema
kuwa ni kweli taasisi yake ilimshikilia na kumhoji mhasibu huyo na sasa
jarada lake tayari limepelekwa kwa Mkurugenzi wa mashitaka (DPP).
‘’Ni
kweli mhasiobu huyo tumemhoji na jarada lake tumelipaleka kwa DPP na
likikamilika tutamfikisha mahakamani pamoja na wenzake akiwemo aliyekuwa
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo’’ alisema Kamanda Mtuka.
Alisema
tuhuma zinazowakabili viongozi hao ni ubadhilifu wa miradi ya Maendeleo
ya wilaya hiyo ambapo kuna dosari zilizojionesha katika upande wa mfuko
wa Afya na Elimu ambapo kwa upande wa Afya pekee Sh. Milioni 101
hazionekani zimeenda wapi na upande wa elimu Sh. Milioni 127.
Uchunguzi
zaidi umebaini kuwa fedha za mfuko wa Afya zinaonekana kutotumika vema
katika Hospitali ya Mission ya Chimala na fedha za elimu kupitia mfuko
wa Capitation Fund zilitakiwa zitumike vema katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa eneo la Ubaruku na rujewa.
Mbali
na viongozi hao, Takukuru imewahoji baadhi ya vigogo wa Halmashauri ya
wilaya ya Ileje na inatarajia kuwahoji wengine kutoka wilaya za Mbeya,
Chunya, Mbozi, Kyela na Jiji la Mbeya kwa tuhuma mbalimbali ambapo
Kamanda Mtuka alisema kuwa ni mapema mno kufafanua jambo hili bali
watakapokuwa tayari wamewahoji atatoa taarifa.
HARARI NA Kalulunga
