| Willy Edward |
ASUBUHI
hii wakati nazungumza na Grace Michael wa NHIF alinipa habari za kusikitisha
juu ya kifo cha Mhariri wa Jamboleo Willy Edward.
Habarui
hizi zilithibitishwa muda mfupi baadaye na mtu ambaye alikuwa naye hadi jioni
jana Mhariri msaidizi wa habari wa Habarileo Joseph Lugendo.
Mtu
mwingine ambaye alikuwa naye mpaka saa 4 usiku alikuwa Martin Malera, wote hao
walikuwa Morogoro hakuweza hata kuelewa nini kinatokea.
Willy
Edward ambaye alikuwa Morogoro kwa mafunzo ya siku moja pamoja na wanahabari ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012 iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu alizaliwa mwaka 1974.
Mmoja wa ndugu wa
marehemu , Catherine Laban , ambaye anamwita Edward, Baba yake ndogo,
alisema , mhariri huyo alifika nyumbani kwao eneo la Forest majira ya saa 4: 30
usiku wa Juni 16, mwaka huu anakoishi mama yake mkubwa ili
kuwajulia hali pamoja na watoto wake wawili wanaoshi hapo.
Kwa mujibu wa ndugu
wa marehemu huyo, mara baada ya kufika na kuwasalimia aliamua
kuwafundisha watoto wake wawili Corman ( 10), na Careb (7) (mtoto wake wa
tatu Caren (3) yupo nyumbani kwao Jijini Dar es Salaam) wanaosoma shule ya msingi hadi saa sita usiku,
ambapo watoto hao walianza kusinzia na hivyo kuwaruhusu waende kulala.
Hivyo aliitisha
Pikipiki ambayo awali ilimleta nyumbani hapo na ikafika majira ya
saa 7:15 usiku ili arejee Hotelini kwake.
Alisema , kabla ya
kupanda pikipiki hiyo, hatua chache aliinama na kushika magoti yake kama mtu
anaye sikiliza maumivu mwilini mwake ,mara akadondoka na kuangukia kichogo.
Hata hivyo, ndugu wa
marehemu hao walisema kuwa , kwa muda mrefu ndugu yao amekuwa akisumbuliwa na
maradhi ya shinikizo la damu (BP).
Kwa upande wake
Mhariri wa Gazeti la Mtanzania , Kulwa Karedia, ambaye aliarifiwa usiku huyo
wakati tukio hilo limetokea, alisema kuwa Marehemu pamoja na Wahariri watendaji
na Wahariri wa habari walifika Mjini Morogoro Juni 15, mwaka huu ili kushiriki
semina ya sensa ya siku moja Juni 16, mwaka huu.
“ Marehemu alikuwa ni
miongoni mwa Wahariri Watendaji walioshiriki semina hii , ambapo baada ya
kumalizika kila mmoja alirejea alikopanga ..lakini usiku saa 5:30 nilipigiwa
simu iliyosema Willy Edward amepata tatizo na nililazimika kwenda kuona tukio
hilo” alisema Mhariri huyo wa Mtanzania.
Alisema baada ya
kufika Hospitalini alikuta tayari Edward amefariki dunia na kuanza
harakati za kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa watendaji wa chombo chake cha kazi
ikiwa na utaratibu za kuomba kibari cha kusafirisha mwili wa marehemu
kurejeshwa Jijini Dar es Salaam kufanyika.
Kwa mujibu wa Mhariri
wa Mtanzania , marehemu kabla ya kuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la JamboLeo ,
aliwahi kufanya kazi Majira akiwa kama Mhariri wa Michezo na baadaye mhariri wa
habari na baadaye kujiunga na JamboLeo.
