VIONGOZI WA AL-SHABAAB KUJADILI JINSI YA KUONDOKA SOMALIA

Upotevu wa kijeshi na tofauti za kiitikadi zimeharakisha baadhi ya viongozi wa al-Shabaab kujadili namna ya kuondoka katika kikundi na kujiunga na mchakato wa kisiasa nchini Somalia na kuachana na mbinu za vurugu za al-Shabaab, kamanda mkuu wa al-Shabaab aliiambia Sabahi.
  • Watuhumiwa wa wanachama wa al-Shabaab wakiwa wamekaa katika lori baada ya kuzungukwa na majeshi ya Somalia wakati wa operesheni ya kuwasafisha wafuasi wa al-Shabaab huko Elasha Biyaha siku ya Jumamosi (tarehe 2 Juni). Kikundi cha al-Shabaab hivi karibuni kimakutwa na upotevu mkubwa, ikiwemo miji ya Afgoye na ngome zao nyingine imara. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]    Watuhumiwa wa wanachama wa al-Shabaab wakiwa wamekaa katika lori baada ya kuzungukwa na majeshi ya Somalia wakati wa operesheni ya kuwasafisha wafuasi wa al-Shabaab huko Elasha Biyaha siku ya Jumamosi (tarehe 2 Juni). Kikundi cha al-Shabaab hivi karibuni kimakutwa na upotevu mkubwa, ikiwemo miji ya Afgoye na ngome zao nyingine imara. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]
Wakati majeshi ya AMISOM na Somalia wanaziteka kambi imara na kushambulia kutoka pande kadhaa, wanachama wa al-Shabaab wamekubwa na migogoro mikubwa ya ndani, makamanda huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema.
Kikundi cha safu ya juu cha makamanda wa al-Shabaab hivi sasa wanakutana katika kijiji cha Jaanale huko Shabelle ya Chini ili kuuandaa kikundi kipya kilichojitenga kwa msaada wa baadhi ya makabila ya Somalia, kikiwa na lengo la kuanza mazungumzo ya kisiasa na maafisa wa serikali ya Somalia baada tarehe ya mwisho Agosti ya kumalizika kwa utawala wa mpito.
Viongozi hao wanaopinga ni pamoja na Sheikh Hassan Dahir Aweys, ambaye karibuni alitoa taarifa ya kuwalaumu viongozi wengine wa al-Shabaab kwa kumwaga damu ya Waislamu na kuua raia wasiokuwa na hatia kwa jina la Uislamu.
Wengine ni pamoja na Sheikh Mukhtar Robow Ali, anayejulikana kama Abu Mansur; Sheikh Mohammed Ibrahim, anayejulikana kama Bilal; Sheikh Hassan Yaqub, mdhamini wa mji wa Kismayo, ambao vikosi vya AMISOM vinasema itaanguka ndani ya wiki zijazo.
Makamanda wengine wa kanda wa al-Shabaab wanaokutana huko Jaanal ni pamoja na: Sheikh Yusuf Isse, anayejulikana kama Kaba-kutukade na mdhamini wa Shabelle ya Kati; Sheikh Mohammed Abdullahi Hirey, anayejulikana kama Sheikh Mohammed Abu Abdalla, mwenye dhamana ya Shabelle ya Chini; Sheikh Yusuf Ali Ugaas kutoka Hiran; Sheikh Ali Mohammed Hussein, kiongozi wa zamani wa al-Shabaab mjini Mogadishu; na Sheikh Abdifatah Mohammed Ali, muweka hazina wa zamani wa Hizbul Islam iliyovunjika.
Makamanda kwa sasa wanamalizia msimamo rasmi wa ushirikiano huo mpya, ambao watautangaza ndani ya wiki chache, kamanda huo wa al-Shabaab alisema.
Alisema kuwa mkutano mwingine unaendelea huko Barawe, Shabelle ya Chini, miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab wenye msimao mkali zaidi. Hawa ni pamoja na: Ahmed Abdi Godane, anayejulikana kama Sheikh Mukhtar Abdirahman Abu al-Zubair, emir wa al-Shabaab; naibu wake, Mahad Warsame Qaleey, anayejulikana pia kama Mahad Karateey; Sheikh Fuad Mohammed Khalaf, anayejulikana kama Fuad Shongole, mdhamini wa ushauri na propaganda; Sheikh Hussein Ali Fiidow, mdhamini wa sera na masuala ya kikanda; Sheikh Ali Mahamoud Rage, anayejuliakana kama Ali Dheere, msemaji mkuu wa kikundi; Sheikh Abdiazziz Abu Musa'ab, msemaji wa kijeshi; and Sheikh Mohammed Hassan Omar, anayejulikana kama Mohammed Abu Abdirahman, ambaye ni kamanda wa Mogadishu.
"Ahmed Godane amekuwa akidharau wito wa kumtaka kuachia ngazi kama kiongozi wa kikundi, kama alivyodai kuwa emir huacha nafasi yake kwa kufa tu, lakini hawezi kujiuzulu,au kulazimishwa kujitoa,” kamanda huyo aliiambia Sabahi. “Hili limepelekea kuweko kwa uasi. Amri zilizotolewa kwa viongozi wetu wawili, Mukhtar Robow na Hassan Dahir, ni kuwamaliza baadhi ya wapiganaji wa kigeni katika kikundi wanaoshutumiwa kwa kufanya ujasusi zilipuuzwa.”
Mwezi Aprili, ripoti ziliibuka kuwa al-Shabaab walimuua mwanajihadi aliyezaliwa Marekani Omar Hammami, anayejulikana kama Abu Mansoor al-Amriki, kutokana na amri kutoka Godane. Ingawaje iliripotiwa kuwa Hammami alionekana yuko hai, al-Shabaab hawakutoa maelezo kuhusu hali yake, kitu kilichochea ripoti za mpasuko mubwa ndani ya kikundi.
Ushirikiano wa al-Shabaab na al-Qaeda pia ulizua upinzani miongoni mwa viongozi wa al-Shabaab, kamanda alisema.
"Pia tulikataa kuwateua wageni kuwa viongozi wakuu, kuunganisha al-Shabaab na al-Qaeda, na kuua watu wasio na hatia bila sababu yoyote ya haki,” alisema. "Tulipinga mashambulizi ya kujitoa muhanga na kuwalenga wananchi na wafanyakazi wa misaada.”