WAZAZI wa wanafunzi wa shule
ya msingi Usoche kata ya Kamsamba
wilaya ya Momba wamelalamikiwa na Mkuu wa shule hiyo kwa kuto
toa ushirikiano na waalimu kwa watoto wao juu ya elimu.
Akizungumza na ELIMTAA mkuu wa
shule hiyo Bw.
Leonard Mwalunda amesema
kuwa wazazi hawaonyeshi
ushirikiano na walimu wa shule
hiyo katika kuiletea maendeleo ya ufauru kwani wanafunzi wamekuwa
wakienda kuchunga ngombe
na kutohudhuria vipindi darasani
Aidha ameongeza
kuwa shule yake haina
walimu wa kutosha, madawati pamoja
na vitendea kazi
ili kuweza kuiletea
maendeleo na ameiomba serikali
itupie macho suala hilo
ili kuinua kiwango
cha taaluma kwa
shule hiyo.
Habari Na Yasinta Msuta
Habari Na Yasinta Msuta
