BABATI: SERIKALI KUAHIDI KUADHIDI KUTATUA CHANGAMOTO HOSPITALINI



WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeahidi kuondoa changamoto kadhaa zinazoikabili wizara hiyo kwa kupeleka vifaa tiba na dawa za kutosha katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya nchini.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Seif Suleiman Rashid, ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi misaada ya vifaa vya hospitali ambavyo vimevyotolewa na Rotary Club wilayani Babati kwa hospitali iliyoko mji mdogo wa Magugu.

Amesema wizara yake pamoja na maeneo mengi ya kutolea huduma za afya zina changamoto hasa kwa upande wa vifaa tiba, hivyo aliahidi wizara kushirikiana na wahisani kama Rotary Club kutoa vifaa hivyo, ili kuhakikisha huduma hiyo inamaliza changamoto zilizopo.