MBUNGE wa Jimbo la Ubungo
John Mnyika ametolewa Bungeni baada ya kutoa kauli chafu na kukataa kuifuta
kitendo ambacho ni kinyume cha kanunu ya Bunge ambayo inamtaka mbunge kufuta
kauli pindi atoapo kauli chafu.
Mnyika ametolewa katika kikao
hicho bunge la bajeti baada ya kutoa kashifa kwa Rais Kiwete kuwa ni dhaifu
pamoja na chama chake kauli ambayo katibu wa Bunge, Job Ndugai akamtaka aifute
na yeye kukataa kuifuta kauli hiyo.
Mnyika kuonyesha msimamo wa
kile alicho kitamka hakutaka kufuta kauli na kisha kutoka bungeni pia Mh.
Ndugai amesema kanunu za bunge ni muhimu kufuatwa kwa wabunge wote na ametolewa
kwa kikao hicho na kuendelea kikao kinacho fuata.
