KICHANGA CHAOKOTWA



MTOTO mchanga amekutwa amefariki duni  baada ya kutupwa pembezoni mwa mto Sinde wa jijini Mbeya.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani, amesema kuwa tukio hilo limetoke jana majira ya 4:00 za asubuhi maeneo ya Sinde.

Kamanda Athumani amesema kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo hajafahamika na mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya pia ameitaka jamii ya jijini hapa kutoa taarika kama kunamtu atakuwa na tetesi za tukio hilo.