WAFANYA biashara
wa soko la
Soweto wamelalamikia uongozi
kutoridhishwa na utendaji wa
kazi katika soko hilo.
Akizungumzia suala
hilo mmoja wa
wafanyabiashara sokoni hapo aliyejitambulisha kwa
jina la Ima Karoti amesema kuwa
hali ambayo ipo
katika soko hilo
ni mbaya kutokana
na kuwa na
choo kimoja pia bomba moja
la maji ukilinganisha
na ukubwa wa
soko hilo,
Kwa upande wake mwenyekiti
wa soko hilo
bwana Mbogela amekiri kuwepo kwa matatizo hayo
na kusemakuwa utendaji
wa halmashauri ndio
chanzo kwani hawatekelezi
majukum yake kwa wakati.
Aidha wafanyabiashara hao
wamesema kuwa bomba
hilo wakati mwaingine
halitoi maji jambo
ambalo pengine linaweza
kuchangia milipuko ya
magojwa kama kipindupindu
na magonjwa mengine,
Bwana Mbogela
amesema kuwa atafanya
mahojiano na halmashauri
ili kuweza kutekeleza
mambo ambayo yapo
kwenye utekelezaji yatekelezwe
kwa wakati.
