WATU WAWILI WAFA KATIKA AJALI MAJINA HAYAJATAMBULIKA

WATU wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 15 kujeluhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kupinduka huko Chiwanda balabala ya Tunduma- Sumbawanga.

Akizungumzi tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athumani
amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majia ya saa 11: 00 jioni  na kutaja namba za usajili wa gari hilo kuwa ni T 289 ACB, T133 aina ya scania  mali ya kampuni ya pepsi.

Pia kamanda Athumani ameongeza kuwa gari hilo lilikuwa linatoka Mbeya na kuelekea Sumbawanga likiwa limebebea soda huku dereva wa gali hilo aliyefahamika kwa jina moja la Masud alikimbia baada ya ajali hiyo kutokea.

Aidha kamanda Athumani amesema kuwa waliofariki hawajafahamika majina yao huku miili yao ikiwa imehidhiwa katika kituo cha afya Ndalambwa na majeruhi wanaendelea na matibabu kituoni hapo.