KENYA:MWANAMAMA AKAMATWA NA SILAHA


Polisi nchini Kenya ilimtia nguvuni mwanamke mmoja mjini Nairobi akiwa na bomu la kurushwa kwa mkono na bastola tatu. 
Maafisa wa polisi wamesema kuwa mwanamke huyo, ambaye jina lake halijatajwa, anashikiliwa kwa tuhuma za kupanga mipango ya ugaidi na anatarajiwa kupelekwa mahakaman wiki hii.
Mkuu wa polisi wa mkoa wa Nairobi, Antony Kibuchi amesema mtuhumiwa amekamatwa katika eneo la Rurii kwenye mashamba ya Zimarmani na anahojiwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi. 
Polisi inajaribu kuangalia kama kuna uwezekano wa kushirikiana na wenzake.