Vikosi vya usalama vya Somalia
vimedai kuwashinda wapiganaji wa al-Shabaab katika mkoa wa Gedo hapo, vikisema
kundi hilo
limepata pigo kubwa.
Hayo yamebainishwa na
Jenerali Abdi Mahdi, mkuu wa vikosi vya Somalia katika mkoa wa Gedo,wakati akizungumza
na mtandao wa habari wa Somalia, wa
Shabelle Media Network.
Maeneo hayo sasa yako chini ya udhibiti wa vikosi vya Kenya na Somalia, amesema jenerali huyo,
akiongeza kwamba vikosi hivyo vya washirika vitarejesha usalama katika mkoa huo
ili kuzuia mashambulizi mengine ya al-Shabaab.
