KUJENGWA ama kutojengwa kwa kivuko cha Mto Songwe
kutategemea matokeo ya utafiti unaofanywa na serikali kwa sasa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge ameliambia Bunge
wakati akijibu swali la Mbunge wa Ileja, Aliko Kibona (CCM), wakati Mbunge huyo
akitaka kujua lini serikali itakuwa tayari kujenga kivuko kwenye mto huo, ili
kunusuru maisha ya raia na mali
zao.
Akijibu swali hilo, Lwenge amesema kabla ya serikali
kufikia uamuzi wa kujenga kivuko kwenye mto huo, wizara itatuma wataalamu
katika mwaka wa fedha 2012/2013 ili kufanya utafiti, ikiwa ni pamoja na kujua
kina cha maji ya kutosha ili kivuko kiweze kuelea wakati wote wa masika na
kiangazi pamoja na upana wa mto.
