DAR: ZIARA YA SIKU NNE YAANZA NI KATIKZ NCHI ZA MAREKANI ULAYA NA BARA ASIA



KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeanza ziara ya siku 14 katika balozi za Tanzania kwenye nchi za Marekani, Ulaya na Asia kukagua namna zinavyotekeleza mambo ya sera na uchumi.

Ziara ya Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa imetangazwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar ers Salaam wakati wajumbe 20 wa Kamati hiyo na makatibu sita wanaondoka nchini.

Hata hivyo, wakati Kamati hiyo ikienda kutembelea balozi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe mwenye dhamana na balozi hizo, amesema ziara hiyo haikuja wakati sahihi, kwa kuwa Mkutano wa Bunge la Bajeti unaendelea.