BRUSSELS: MPANGO MKAKATI WAWEKWA NA VIONGOZI WA UMOJA WA ULAYA

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameweka mpango mkakati wa miaka 10 kwa ajili ya kuimarisha uchumi ikiwa ni hatua ya awali kuelekea mkutano wa kilele wa umoja huo mjini Brussels utakaoanza kesho. 

Mpango huo unatoa wito kwa nchi 27 mwanachama wa umoja huo kukubali uamuzi wa mamlaka kwenye masuala ya fedha, bajeti na sera za uchumi  kuhamishiwa kutoka miji yao mikuu hadi  mjini Brussels katika kipindi cha miaka 10 ijayo. 

Wakiwa chini ya shinikizo kutoka kwa washirika wenzao wa nchi za kundi la G20, nchi za Umoja wa Ulaya zinapambana ili kupata njia muafaka ya kuutatua mzozo wa kiuchumi  katika kanda ya sarafu ya Euro.